Scroll To Top

Kuamini Uchumi Wa Mungu

Sehemu ya Nne

Na Jacquelyn Fedor

Ilitafsiriwa Na William Obura
2022-04-25


Tafadhali bofya maandishi ya samawati hafifu kwa maelezo zaidi


TAZAMA KWA KINA NCHI YA AHADI NA UZAO WA IBRAHIMU


Leo watu wa Mungu wako tena katika aina fulani ya nyika kama Israeli ya zamani, lakini wakati huu ni nyika ya ulimwengu wa Adamu. Majangwa yaliyoundwa na uchumi wa mwanadamu na matunda mabaya ya mifumo yao ya kiakili, sasa yanaanza kutuathiri sisi sote. Bado, ahadi ziko mbele yetu. Mungu, na uzima ndani ya Ufalme Wake wa milele, ni nchi yetu ya ahadi. Je, tutachukua njia ndefu huko kama walivyofanya Israeli ya zamani? Je, tutasisitiza kufanya mambo kwa njia yetu, kwa njia ya Hawa, na kumweka Mungu mipaka? Au tutaingia katika pumziko la Mungu, na kufanya mambo kwa njia Yake? Je, tunaweza kumwacha Roho aongoze na kuruhusu mipango na njia za Mungu, uchumi wake, kutiririka kupitia kwetu? Ni vita katika akili zetu. Je, tunaweza kuwa watoto waliojawa na imani, wenye kutumainia wa Siku Mpya ambao wana sehemu katika kuona ulimwengu ukirejeshwa kwa njia za Ufalme wa Mungu? Au, tutadai njia za zamani, njia za ulimwengu, kulingana na ujuzi kutoka kwa Mti wa Mema na Uovu, kwa sababu zinaleta maana zaidi kwetu? Je, tunapanda katika shamba la nani kwa uaminifu? Tuna haki ya kuchagua kubaki katika Ukristo kama Adamu na kupanda wakati, juhudi, na fedha kwenye mashamba hayo, au tunaweza kuwa wa Yoshua na Kalebu tukiwa na roho tofauti na kuwa watu wanaopanda tu katika mashamba ya Ufalme Kwa mfano, wafanyabiashara wa Mungu wanapaswa kutoogopa mipaka mipya, na kuanza kutumainia uchumi wa Mungu. Wanapaswa kutumainia maisha yao kwa hekima kwa Yule asemaye katika Hagai 2:8, “fedha yote ni yangu na dhahabu ni yangu, na kuwa watiifu kwa sheria za kiroho zinazoongoza fedha ndani ya Ufalme wa Mungu. Tena, ni chaguo la mtu binafsi hata hivyo. Tunatumahi, kwa ajili ya mwili mzima, tutafanya uamuzi sahihi, na hivyo kubarikiwa na kupewa fedha za kusaidia kurudisha mipango ambayo Mungu anayo kwa ajili ya familia yake, kuruhusu ushindi utimie. Fikiria jambo hili, ikiwa tunajaribu kutembea katika ulimwengu wa Adamu tukiwa na kanuni za Ufalme wa kimungu, je, unafikiri Shetani atatubariki? Au tukijaribu kutembea katika Ufalme wa Mungu, lakini tukiishi kupatana na kanuni za Shetani, je, unafikiri Mungu atatubariki? Vyovyote vile, tusingekuwa katika. Au njia bora ya kusema itakuwa; tusingekuwa ardhi ya mtu pekee. Mungu anasema sisi ni nchi yake, shamba lake, ambalo alilipa kwa maisha yake. Ikiwa hatujakiri kabisa umiliki Wake, Shetani atachukua fursa ya mtazamo wetu wa kutofanya maamuzi na ukosefu wa shukrani ili kutumeza. Mungu huwalinda walio Wake pekee, wale wanaofanya kazi pamoja Naye kujenga Ufalme Wake.
1 Wakorintho 3:9
9 Maana sisi ni wafanyakazi pamoja na Mungu; nyinyi ni shamba la Mungu, nyinyi ni jengo la Mungu.
Unaona, tumeumbwa kwa udongo na uhai wa Mungu uliopuliziwa ndani yetu. Unaweza kusema tunaishi ardhini. Tayari dunia imefunikwa na tani nyingi za watu wa Shetani ili kufanyiza ulimwengu kama tunavyoujua sasa, na sisi wakati fulani tulikuwa sehemu ya uchafu. Lakini, Yesu alitununua tena, na akatufanyia jubilee, ama akatuweka huru. Dunia inapofunikwa au kuwekwa upya na watu wa Mungu, dunia mpya au iliyorudishwa itaonekana. Ustaarabu wa zamani hatimaye utafunikwa. Isaya alitabiri juu ya hili ni Isaya 61. Tusome kidogo tu kuanzia mstari wa
Isaya 61:4, 7, 11
4 Nao (watoto wa Mungu) watajenga upya magofu ya kale, na watainua ukiwa wa kwanza. nao wataitengeneza miji iliyoharibiwa, ukiwa wa vizazi vingi.
7 Badala ya aibu yenu mtapata heshima maradufu, na badala ya kuchanganyikiwa watafurahia sehemu yao. Kwa hiyo katika nchi yao watamiliki maradufu (maagano yote mawili ni ya uzao wa Ibrahimu); furaha ya milele itakuwa yao.
11 Kwa maana kama vile nchi itoavyo chipukizi yake, kama bustani itoavyo vitu vilivyopandwa ndani yake, ndivyo Bwana MUNGU atasababisha haki na sifa kuchomoza mbele ya mataifa yote.
Ikiwa wewe ni mpokeaji wa Wagalatia 3:28, tafadhali rudi nyuma na usome sura nzima. Uumbaji wote unangojea kwa hamu hii. Kumbuka, ushindi kwa nchi ya kupendeza, Hephziba, ulipatikana kabla ya kuwekwa msingi wa dunia. Ni "mpango uliokamilika". Uchumi wa Mungu hakika utashinda uchumi wa Shetani.
Isaya 62:4-5 inasema:
4 Hutaitwa tena, Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, “Ukiwa”; lakini utaitwa Hefsiba, na nchi yako Beula; kwa kuwa BWANA amependezwa nawe, na nchi yako itaolewa.
5 Maana kama vile kijana amwoavyo msichana bikira, ndivyo wanao watakuoa wewe; na kama vile bwana arusi anavyomfurahia bibi-arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.
Sisi, kama nchi yake, tutaolewa na Bwana, ambaye ni nchi yetu ya ahadi, na kuunganishwa pamoja, sisi ni Ufalme, sisi ni Simchat Torah, sheria zake, sisi ni familia ya kweli ya Mungu. Sisi ni Beulah, tulioolewa. Je, tunayo imani ya kuyaondoa haya? Je, kweli tunanyenyekea kwa Mungu? Je, tunaweza kuondokana na mawazo yetu ingawa mambo yanaweza kuwa magumu sana, hata kuonekana kuwa haiwezekani. Je, sisi ndio tunaoweza kuliyumbisha na kulivuta kanisa kutoka katika mitego ya Shetani na Babeli, ambazo zimekaribia kuuteketeza kabisa Ukristo, na kuwaongoza watu wa Mungu hadi hatua inayofuata? Ikiwa tuko, basi ni muhimu kwamba tuelewe, kwamba kama vile uchumi ulivyoanzishwa tena mwanzoni mwa Ukristo, vivyo hivyo lazima uimarishwe tena katika mapambazuko ya kanisa la ushindi, kanisa la milele. Tunaweza kufanya hivyo, tuna uwezo wa kuiondoa, sisi ni uzao wa Ibrahimu. Baba Ibrahimu alikuwa na imani na matendo yake yalithibitisha hilo. Yetu pia inapaswa.
Yakobo 2:21-24
21 Je! Abrahamu baba yetu hakuhesabiwa haki kwa matendo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? (Fikiria juu ya hili, na ukizungumza juu ya somo la fedha, unaweza kutoa pesa zako za ziada, yai la kiota chako, kwenye ghala ili litumike jinsi Mungu anavyoona inafaa? Je, unaweza kumwachilia mtoto wako mchanga?)
22 Waona, kwamba imani yake iliandamana na matendo yake, na imani ilikamilishwa kwa matendo?
23 Na maandiko yakatimia yaliyosema: "Abrahamu alimwamini Mungu,na ikahesabiwa kwake kuwa mwadilifu." Naye aliitwa rafiki wa Mungu. (Alimruhusu Mungu kushikilia uhai wa mtoto wake mikononi Mwake, hakuna swali lililoulizwa. Je! ni lazima uwe na udhibiti wa hatima ya pesa zako, au unaweza kuzileta ghalani, bila swali lolote?)
24 Unaona? basi, mtu huhesabiwa haki kwa matendo, wala si kwa imani pekee.
Ni lazima tuzingatie mambo haya, kwa sababu yote tuliyojifunza hapo awali yamefundishwa moja kwa moja kutoka kwa Mti wa Mema na Maovu na njia zetu, njia za zamani, si njia za Mungu. Bila kujua, Shetani anaweza kuwa ametengeneza mawazo yetu kwa kadiri ambayo kwa kweli tumekuwa adui wa mipango ya Mungu. Kwa hivyo, ikiwa tunadai kuwa sehemu ya watoto wa Mungu, kama msemo unavyosema, na tuweke pesa zetu mahali pa mdomo wetu, na "matendo yetu mahali ilipo imani yetu"! Kweli tuwe watu wa imani, tupande muda na fedha katika ardhi yake Mungu anavyotupa mbegu ili tuwekeze. Tunahitaji kufanya mpira uendeshwe, kwa njia ya mfano, ili kuonyesha jinsi njia ya Mungu inavyoweza kufanya kazi kikweli. Bwana anaendelea kusema “ni siku mpya na kuna njia mpya” katika wimbo wa Bwana. Je, kweli tulifikiri uelewa wetu wa sasa wa fedha ungebaki kama ilivyo sasa? Kila kitu kingine tulichofundishwa ulimwenguni hakikuwa sahihi, kwa sababu tulifanya kazi kupitia ujuzi wa Mti wa Mema na Ubaya kama wazao wa Hawa. Kwa hiyo, jambo la maana kama uchumi lingewezaje kuepuka usikivu wa Shetani? Lakini unajua nini, watoto wa kweli wa Abrahamu watakuwa washindi. Amosi alitabiri juu ya wakati ambapo baraka za Ufalme zingekuwa nyingi sana, na nchi ingezaliana haraka sana, hivi kwamba ingekuwa vigumu kutofautisha mzunguko mmoja kutoka kwa mwingine. Mmoja angekuwa akipanda huku mwingine akivuna kwa hiyo hapakuwa na upungufu, kwa sababu walishiriki katika mambo yote. Ni “njia” ya Mungu. Anatamani sisi tuwe na tele, tuishi kwa wingi, na tuwe na tele kwa hali zote. Wakati mambo yanaporekebishwa, na kuletwa katika mstari na sheria ya kiroho kupitia ujuzi kutoka kwa Mti wa Uzima, “ndipo” Yeye atammeza adui anayeng’oa mbegu zetu, au apandaye magugu mengi sana hivi kwamba mbegu njema inasongwa. Wakati huo biashara za Israeli zitasitawi, na watu Wake wataishi katika utele ulioahidiwa, wanapokuwa huru kutoka kwa mawazo yao na kuwa tayari na watiifu kuishi kwa kanuni za Ufalme.
Isaya anasema katika Isaya 1:19
19 Kama mkikubali na kutii mtakula mazao mema ya nchi;
Sisi ni shamba lake, na ikiwa kwa hiari tutashiriki yale ambayo yametolewa kupitia sisi kwa sisi, kwa kuweka ghala imejaa, hakutakuwa na haja kati yetu. Hii haitatokea mara moja, kwani tumekuwa tukifanya vibaya kwa muda mrefu. Itachukua muda kugeuka. Acheni tusome unabii unaopatikana katika Amosi 9:13-15 andiko ambalo tulirejelea hapo awali, kwa sababu ni picha ya wazi ya usalama na uthabiti wa Ufalme wa Mungu kwa wale ambao watajifunza kutegemea uchumi wa Mungu.
Amosi 9:13-14
13 Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo mkulima atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu;
Kwa maneno mengine, mvunaji na mkanyaga zabibu atashiriki pamoja na wale wanaopanda. Kwa hivyo kuwe na chakula na divai kwa wale walio katika hatua za mwanzo za kupanda. Vivyo hivyo, wakati mvunaji na mkanyagaji wa zabibu wanapanda tena mazao yao, mpanzi atatoa. Hakutakuwa na nyakati za kiangazi tena bila riziki kwa mtu yeyote. Milima itadondosha divai tamu, na vilima vyote vitatiririka nayo. 14 Nitawarudisha mateka wa watu wangu Israeli, (walio naswa katika ulimwengu na Babeli); Wataijenga miji iliyoharibiwa na kukaa ndani yake (biashara zao zitafanikiwa kadiri wanavyopanda katika Ufalme na Ufalme utaongezeka wenyewe); Watapanda mizabibu na kunywa divai yake; Nao watatengeneza bustani na kula matunda yake.
Kutakuwa na siku ambayo watu wa Mungu watakuwa na ufanisi mwingi zaidi, na maisha kwa wingi, kwa sababu tu wanapanda katika mashamba ya Mungu, ambao nao watashiriki mavuno yao kwa furaha pamoja nao. Haya ndiyo maisha mazuri na kufanya biashara katika Ufalme wa Mungu. Hivi ndivyo tunavyofanikiwa. Pia, tunapomiliki nchi, au kuleta mabaki na kupanda mbegu za ukweli ndani yao, huu ni mfano wa ardhi ya Mungu inayozaa mazao mapya, vito vipya, hazina Zake na haya yanakuwa ardhi ya baadaye na wao wenyewe wazaliaji. Tukizidisha kwa ajili ya Bwana, Yeye hufanikiwa nasi tunafanikiwa.
Kwa hiyo kabla ya kufunga, hebu turudie yale tuliyojifunza. Kwanza, sisi ni nchi ambayo Ufalme utasimamishwa ndani yake, kama udongo mzuri wa juu, na tunapaswa kuwa sheria inayouongoza. Sisi ni sheria juu ya mizani isiyo ya haki, kuiba, kudanganya, mbinu zote za biashara za kidunia. Mbili, tunapaswa kupendana kila mmoja na kushiriki kana kwamba tumeolewa sisi kwa sisi, na kwa hiyo tuwe nchi moja na Mungu. Tatu, tunapaswa kufanya biashara tukifikiria kanuni za Ufalme wa Mungu, kwa kutii mwongozo wa Bwana, ingawa njia ya Mungu ni tofauti kabisa na jinsi tulivyoifanya duniani. Roho Mtakatifu ataongoza badala ya akili zetu. Tunapojifunza kuishi kupitia mawazo ya Mungu, moja kwa moja tutafanya mambo kwa njia yake. Nne, ni lazima tuujenge Ufalme wake, si ule wetu binafsi. Yake ni yetu hata hivyo, ili tuweze kutembea kwa imani tukijua hili, tukiamini hili, na kuwa na ujasiri wa kulifanyia kazi. Na tano, leteni ziada kwenye ghala ili wale aliowachagua kugawa wafanye hivyo. Vinginevyo unakuwa kizuizi kwa mtiririko wa kiuchumi wa Mungu. Malaki alitabiri matokeo ya utayari wetu wa kutembea kulingana na uchumi wa Mungu katika Malaki 3:12.
Malaki 3:12
12 Na mataifa yote watawaiteni waliobarikiwa; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana,” asema BWANA wa majeshi.
Bofya vichwa ili kucheza nyimbo zinazohusiana na mada hii
The Appearing Of The Children Of God
Abraham's Seed
The Church Triumphant